Matokeo ya ligi kuu England

Katika mchezo uliotangazwa kupitia Idhaa ya Kiswahili ya BBC Aston Villa imetoka sare ya 1-1 dhidi ya Bolton Wanderers. Goli la Aston Villa limefungwa na Ashley Young katika dkika ya 13. Goli la kusawazisha la Bolton limefungwa na Kevin Davies dakika ya 35.

Blackburn Rover nayo imetoka sare ya 1-1. Christopher Samba alifunga bao la Rovers, huku bao la kusawazisha likifungwa na Clint Dempsey dakika ya 56.

Newcastle imeizaba Everton kwa bao 1-0. Everton ikicheza kwao ilishindwa kutamba na kupoteza mchezo huo kwa goli pekee lililofungwa na Hatem Ben Arfa katika dakika ya 45.

Mapema Stoke City waligawana pointi na West Ham kwa ktoka sare ya 1-1. West Ham waliandika bao lao kupitia Scott Parker katika dakika ya 32 huku bao la kusawazisha la City likifungwa na Kenwyne Jones dakika ya 48.

Tottenham imeiangushia kisago cha magoli 3-1 Wolves. Wolverhampton ndio ilikuwa ya kwanza kuona lango la Spurs kupitia Stephen Fletcher dakika ya 45. Rafael Van Der Vaart alipachika bao la kwanza kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 77. Dakika 10 baadaye Roman Pavlyuchenko aliandika bao la pili na Alan Hutton kuandika bao la tatu katika dakika ya 90.

West Brom nayo imeichapa Birmingham City kwa mabao 3-1. Magoli ya West Brom yamefungwa na Peter Odemwingie, Jonas Olsson na Scott Dann aliyejifunga. Bao pekee la Birmingham limefungwa na Cameron Jerome.