Uchunguzi wa ubakaji wakamilika DRC

Image caption Ubakaji wachunguzwa Congo

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo inasema matokeo ya awali ya uchunguzi wa hivi karibuni kuhusu visa vya ubakaji mashariki mwa nchi hiyo yatachapishwa siku chache zijazo.

Waziri wa sheria wa Congo Luzolo Bambi amesema mahakama ya kijeshi imeanzishwa kuwashtaki washukiwa wa matukio mia moja hamsini ya unyanyasaji wa jinsia.

Bwana bambi Lessa ameliambia baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva kwamba nchi yake imeazimia kuwaadhibu wahusika na ghasia za ubakaji.

Kauli yake imekuja siku mbili baada ya msemaji wa serikali ya Kongo lambrt mende kupinga ukosoaji wa baraza la usalma l Umoja wa mataifa kuhusu namna Congo ilivyoshughulikia ripoti za ubakaji mkubwa nchini humo.