Somalia: Kasri la rais lashambuliwa

Image caption mlipuaji wa kujitoa mhanga ashambulia kasri ya rais

Mlipuaji bomu wa kujitolea mhanga nchini Somalia amejilipua katika lango la kasri ya rais katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Maafisa nchini humo wame walaumu wapiganaji wa Al Shabaab kuhusika na shambulio hilo, lililofanyika wakati msafara wa wanajeshi wa kulinda amani walipokuwa wakiingia kwenye eneo hilo.

Mapema mwezi huu mlipuaji wa kujitolea mhanga wa Al-shaabab aliushambulia uwanja wa ndege wa Mogadishu na kuwauwa watu kadhaa wakiwemo askari wa wawili wa kulinda amani wa muungano wa ulaya.