Rais wa Somalia aomba msaada zaidi - UN

Rais wa Somalia
Image caption Rais wa Somalia

Rais wa Somalia, Sharif Sheikh Ahmed ameliomba baraza kuu la Umoja wa Mataifa kusaidia serikali yake ya mpito na pia juhudi zake za kuleta uthabiti nchini humo.

Rais Ahmed pia ametoa wito kwa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio litakalosaidia kuzuia kusambaa wa mitandao ya Al Qaeda, na makundi mengine ya wapiganaji wa kiislamu kama vile Al Shabaab.

Akihutubia baraza kuu la Umoja huo mjini New York, rais Ahmed alikariri haja ya kutatua kwa dharura matatizo ya kisiasa na kiuchumi yanayokumba Somalia.