Mwanawe Kim Jong-il ateuliwa Generali

Kim Jong-Un

Shirika la habari la Korea Kaskazini limesema mtoto wa kiume wa mwisho wa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Il, ameteuliwa kuwa Jenerali wa ngazi ya juu katika jeshi la nchi hiyo.

Ni mara ya kwanza kwa jina la Kim Jong Un ambaye anadhaniwa anakaribia umri wa miaka thelathini, kuchapishwa na vyombo vya habari nchini humo, licha ya kuongezeka kwa fununu kuwa kiongozi wa nchi hiyo anamwandaa mwanawe kumrithi.

Mwandishi wa BBC nchini Korea Kusini amesema ikiwa Kim Jong Un atateuilwa kuwa mmoja wa maafisa wakuu wa chama wakati wa mkutano wa baraza kuu la chama hicho ambao unaanza hivi karibuni, itakuwa ni ishara kuwa Korea Kaskazini inanuia kuendeleza utawala wa kurithishana kuelekea kizazi cha tatu cha familia hiyo.