Gaza: Mahmoud Abbas akutana na PLO

Image caption Rais wa Palestina Mahmoud Abbas

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas hii leo atafanya mashauriano na na viongozi wa PLO juu ya mustakabal wa mazungumzo ya amani na Israel ambayo yamekwama kutokana na mtafaruku juu ya ujenzi wa makazi ya walowezi wa kiyahudi katika ukingo wa magharibi.

Wajumbe wa Palestina katika mashauriano hayo wametishia kujiondoa iwapo Israel haitaongeza marufuku ya ujenzi huo.

Marufuku iliyowekwa awali na Israel juu ya ujenzi huo yalikwisha yapata wiki moja iliyopita.

Wajumbe kutoka Marekani na Jumuiya ya Ulaya nao wamekuwa wakiyashawishi makundi yote mawili katika mashaurinao hayo waafikiane juu ya suala hilo lakini hadi sasa hakuna matumaini kabisa.