Nigeria: Mshukiwa wa bomu akamatwa SA

Image caption Bendera ya Nigeria

Kiongozi wa zamani wa kundi la waasi nchini Nigeria ametiwa nguvuni kuhusiana na mashambulio ya bomu nchini Nigeria ya Ijumaa iliyopita.

Henry Okah alikamatwa na maafisa wa polisi wa Afrika Kuisni katika nyumba yake mjini Johannesburg. Okah aliwahi kuwa kiongozi wa kundi la MEND kundi la waasi lililofanya mashambulio mengi dhidi ya maeneo ya mafuta.

Kundi hilo limedaiwa kuhusika katika mashambulio hayo japo lilikuwa linastahili kutekeleza usitishwaji wa vita chini ya makubaliano kati yake na serikali.