Wamiliki wapya Liverpool "kufuta madeni"

Wapya
Image caption Wamiliki wapya

Wamiliki watarajiwa wa klabu ya Liverpool, wameahidi kuondoa madeni yote ya timu hiyo ya ligi kuu ya England, wakati watakapoichukua rasmi klabu hiyo.

Wamiliki hao, kampuni ya New England Sports Venture (NESV) ya Marekani wametoa taarifa inayosema itaondoa "deni lote la mapato" kutoka katika klabu hiyo iwapo ombi lake la Pauni milioni 300 litakubaliwa.

NESV, ambayo pia humiliki timy ya mchezo wa baseball ya Boston Red Sox, imethibitisha kuwa ombi lake limekubaliwa na bodi ya wakurugenzi ya Liverpool.

Lakini wamiliki wa sasa wa Liverpool Tom Hicks na George Gillett wanajaribu kuzuia uuzwaji wa klabu hiyo, wakisema hatua hiyo inaishusha thamani klabu.

Hicks na Gillett wanajaribu kubadili mkurugenzi mkuu Christian Purslow na mkurugenzi wa biashara Ian Ayre, kwa kuwapa nafasi hizo Mack, mtoto wa Hicks na mshirika mwenzao wa biashara Kay McCutcheon.

Hivi sasa Purslow, Ayre na Martin Broughton mwenyekiti wa Bodi, wanawasiliana na wanasheria wao kuona kama wanaweza kuzuia jitihada za wamiliki kuwaondoa, na pia kufanikisha uuzwaji wa timu hiyo kwa wamarekani wa NESV.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii