Liverpool kuuzwa

Bodi ya klabu ya soka ya Liverpool inayocheza ligi kuu ya England, imekubali kuiuza klabu hiyo kwa kampuni ya kimarekani iitwayo New England Sports, ambayo pia inamiliki timu ya Boston Red Sox nchini Marekani.

Image caption 'Katu hutokuwa peke yako'

Red Sox ni timu ya mchezo wa baseball.

Makubaliano haya yamefikiwa kufuatia tofauti kuzuka baina ya wajumbe wa bodi ya Liverpool, na kuhusisha wamiliki wa klabu hiyo Tom Hicks na George Gillett.

Wamiliki hao walijaribu kuzuia kufanyika kwa mauzo ya klabu hiyo, lakini wakazidiwa nguvu ya kura na wakurugenzi wengine wa Liverpool.

Mwenyekiti wa Liverpool Martin Broughton amesema klabu hiyo italazimika kupitia masuala kadhaa ya kisheria ili kufanikisha mauzo ya klabu hiyo.

Bado haifahamiki iwapo Liverpool itanunuliwa kwa kwa njia za kawaida, au italazimika kupitia hatua ya mfilisi kwanza.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii