Wafanyakazi Ufaransa kuandamana . kupinga kunguzwa kwa pensheni

Vyama vya wafanyakazi nchini Ufaransa vinaandaa migomo zaidi hii leo kupinga mpango wa Rais Sarkozy wa kupunguza malipo ya pensheni.

Huduma za usafiri wa anga na wa mabasi ya umma zinatarajiwa kuvurugwa. Wanafunzi wa shule na vyuo pia wanatakiwa kushiriki katika maandamano mitaani.

Hii ni siku ya tatu ya mgomo wa pensheni nchini Ufaransa katika kipindi cha mwezi mmoja.

Serikali ya Ufaransa imeongeza muda wa kustaafu kufikia miaka 67 ili kupata pensheni kamili.