Nchi nne za Kiafrika kupambana na LRA

Joseph Kony
Image caption Joseph Kony

Muungano wa Afrika umesema nchi nne zinaunda kikosi cha pamoja cha kupambana na kundi la waasi la Lord's Resistance Army.

Hatua hii ni sehemu ya juhudi za Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Uganda ili kuzidisha shinikizo dhidi ya LRA ambalo ni kundi lililoundwa nchini Uganda miaka ishirini iliyopita.

Umoja wa Mataifa umesema kundi hilo limesababisha watu laki nne kukimbia makaazi yao katika miaka miwili iliyopita, na linashambulia miji na vijiji vilivyo mbali ya kilometer elfu moja kutoka makao yao ya asili.