Kesi dhidi ya Bemba kuamuliwa leo na ICC

Image caption Hatma ya kesi dhidi ya Bemba kuamuliwa na mahakama ya ICC

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, hii leo itatoa uamuzi kama kesi aliyofunguliwa aliyekuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Jean Pierre Bemba katika mahakama hiyo itaendelea.

Bemba alikuwa ameiomba mahakama hiyo ya rufaa kutupilia mbali mashtaka yaliyoletwa dhidi yake kuwa aliamrisha vitendo vya uhalifu wa kivita katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kati ya mwaka 2002 na 2003.

Mawakili wake wanadai kwamba tayari madai dhidi yake yanachunguzwa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na hapaswi kufungulia kesi nyingine kuhusiana na madai hayo.

Bw. Bemba alikamatwa nchini Ubelgiji mwaka 2008 na kupelekewa the Hague, Uholanzi.