Pweza mtabiri Paul amekufa

Pweza aliyepata umaarufu mkubwa wakati wa mashindano ya kuwania Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini amekufa.

Image caption Pweza Paul amekufa

Samaki huyo alibashiri matokeo ya mechi zote za Ujerumani nchini Afrika Kusini na baadaye ushindi wa Hispania.

Baada ya mashindano ya Kombe la Dunia pweza Paul alitokea kwenye video akiipigia debe Uingereza kuwa mwenyeji wa kombe la dunia ya 2018.

Kulingana na hifadhi ya Oberhausen nchini Ujerumani, kifo cha pweza huyo aliyepewa jina Paul ni cha kawaida.

Pweza Paul ambaye alikuwa maarufu sana katika mashindano ya Kombe la Dunia kwa kutabiri sawasawa matokeo ya mechi za timu ya taifa ya Ujerumani nchini Afrika Kusini na pia mechi ya fainali, katika utabiri wake wa mwisho alikuwa akionesha England itakuwa na nafasi ya kuandaa Kombe la Dunia mwaka 2018.