Ratiba Carling Cup robo fainali yatolewa

Manchester United itatetea taji la Kombe la Carling hatua ya robo fainali kwa kusafiri hadi Upton Park kupambana na West Ham.

Image caption Carling Cup robo fainali

Pambano jingine la robo fainali, litakuwa Birmingham dhidi ya Aston Villa watakaomenyana katika uwanja wa St Andrew.

Arsenal wanaopewa nafasi kubwa ya kunyakua Kombe hilo tangu mwaka 2005 mara ya mwisho kunyakua Kombe, watawakaribisha Wigan katika uwan ja wao wa Emirates.

Timu ya Ipswich, ambayo pekee haichezi Ligi Kuu ya England iliyosalia katika mashindano hayo, watawakaribisha nyumbani West Brom.

Arsenal, iliyoilaza Newcastle 4-0 katika mchezo wa raundi ya nne, watawakaribisha Wigan waliongia hatua hiyo baada ya kuwalaza Swansea mabao 2-0.

Manchester United waliowatoa katika mbio za kuwania Kombe la Carling Wolves siku ya Jumanne kwa mabao 3-2, itataka kuweka nguvu zaidi kuelekea uwanja wa Wembleya kwa fainali mara watakapomaliza ziara ya Upton Park.

West Ham iliishinda Stoke City katika muda wa nyongeza na kwa sasa ndio wanaburura mkia wa Ligi Kuu ya England wakiwa na rekodi mbaya wanapokutana na Manchester United kwa kufungwa katika mechi sita zilizopita, wakiwa wamefunga bao moja tu na kufungwa 17.

Kwa Birmingham, waliowatoa Brentford kwa mikwaju ya penalti na Aston Villa itakuwa ni nafasi yao nzuri kufufua upya upinzani wao wa jadi watakapokutana katika mchezo wa Ligi Kuu ya England siku ya Jumapili.