Uchaguzi wa urais waanza nchini Ivory Coast

Shuguli ya kupiga kura inaendelea nchini Ivory Coast katika uchaguzi wa urais ambao ulikuwa umehairishwa mara sita

Image caption Waziri Mkuu wa Ivory Coast

Awali, waziri mkuu wa nchi hiyo, Guillaume Soro, alisema uchaguzi huo wa urais utakuwa huru na waki.

Takriban wapiga kura milioni sita wanashiriki katika zoezi hilo la kumchagua rais mpya.

Uchaguzi huo unatarajiwa na wengi kuwa utaliunganisha taifa hilo lililogawanyika baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2002.

Kuna wagombea kumi na wanne wa kiti cha Urais akiwemo rais wa sasa, Laurent Gbagbo.

Miongoni mwa wanasiasa wanaotarajiwa kuumpa Bwana Gbagbo ushindani mkali ni pamoja na Alassan Ouattara na Henri Konan Bedie.

Waziri huyo mkuu mkuu ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa kundi la waasi ametoa wito kwa wagombeaji wote kuwa tayari kukubali matokeo ya uchaguzi huo.

Mwandishi wa BBC mjini Abidjan anasema wapiga kura wengi wameelezea wasi wasi wao kuhusu hali ya usalama nchini humo ikiwa wagombeaji wa kiti hicho hawatakubali matokeo ya uchaguzi huo.

Ivory Coast ni mojawapo ya mataifa yaliyokuwa yamepiga hatua kubwa barani afrika kabla ya kutokea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2002.