Ugaidi: Watu 2 wanaswa nchini Yemen

Maafisa wa Ulinzi wa Yemen
Image caption Maafisa wa Ulinzi wa Yemen

Maafisa wa ulinzi nchini Yemen, wanaendelea na msako wa kuwatafuta watu waliotuma vifurushi viwili vya mabomu vilivyonaswa katika ndege mbili za kubeba mizigo nchini Uingereza na Dubai siku ya ijumaa.

Mwanafunzi mmoja wa kike wa chuo cha matibabu katika mji mkuu wa Yemen Sanaa, amekamatwa pamoja na mama yake baada ya polisi kuzingira nyumba yao.

Wakili wa mwanafunzi huyo amesema mteja wake hana hatia na kwamba alihadaiwa, kuacha anwani yake katika vifurushi hivyo.

Vifurushi hivyo vilikuwa vikisafirishwa hadi marekani ili kupelekwa katika maeneo mawili ya maabadi ya kiyahudi katika jimbo la Chicago.