Mawaziri wa Kikwete watupwa nje

Matokeo ya awali katika uchaguzi wa wabunge nchini Tanzania yanaonyesha kuwa mawaziri wasiopungua watatu waliokuwa katika serikali iliyomaliza muda wake tayari wameshapoteza viti vyao vya ubunge.

Aliyekuwa Waziri wan chi katika ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia mazingira, Dr Batilda Buriani wa CCM ameangushwa na Godbless Lema wa CHADEMA katika jimbo la Arusha mjini.

Lawrence Masha, aliyekuwa Waziri wa mambo ya ndani, amepigwa mwereka katika jimbo la Nyamagana na mgombea Ezekiah Wenje pia wa chama cha CHADEMA.

Ingawa CCM imeonyesha uimara wake katika maeneo mengi ya nchi, imeonekana kupoteza viti ambavyo awali vilikuwa ni ngome ya CCM.

"Kigogo" mwingine aliyepigwa mwereka ni Getrude Mongella wa CCM katika jimbo la Ukerewe, aliyewahi kuwa spika wa Bunge la Afrika.

Vincent Nyerere ambaye ni ndugu wa damu wa rais wa kwanza wa Tanzania, Julius Nyerere, ameshinda jimbo la Musoma mjini.

CHADEMA imeendelea kuipokonya viti CCM, ambapo katika jimbo la Iringa mjini Peter Msigwa amemshinda Monica Mbega.

Wengine wa CHADEMA ni John Shibuda, Maswa Magharibi.

Sylvester Kasurumbai - Maswa Mashariki

Pia chama cha wananchi CUF (Civic United Front) kimetwaa jimbo la Lindi mjini ambako Salum Baruan.

Hata hivyo CCM imeshinda kwa idadi kubwa ya kura katika ngome zake kama vile Peramiho, Jenista Mhagama amepata zaidi ya asilimia 90 ya kura.

Mohammed Dewji - Singida Mjini.

Mtutula Abdallah Mtutula – CCM - Tunduru Kusini.

Matale Ramo – CCM - Tunduru Kaskazini.

Abdulkarim Shah wa CCM ameibuka kidedea katika jimbo la Mafia.