Sudan Kusini na Kaskazini zashutumiana

Jeshi la Sudan Kusini limeshutumu jeshi la Sudan Kaskazini kwa kuwashambulia wanajeshi wake na kukiuka mkataba wa amani uliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo mwaka wa 2005.

Image caption Wanajeshi wa Sudan Kusini

Msemaji wa SPLA Kuol Diem Kuol amesema mwanajeshi wake mmoja alijeruhiwa kwenye shambulio lililofanywa na wanajeshi wa kaskazini katika jimbo la Upper Nile.

Mwandishi wa BBC nchini Sudan amesema hali ya taharuki inaendelea kutanda huku taifa hilo likijiandaa kupiga kura ya kuamua kuhusu uhuru wa eneo la Kusini mwezi wa Januari mwakani.