Mshukiwa wa mabomu aachiwa huru Yemen

Serikali ya Yemen imemuachilia huru mwanafunzi mmoja Hanane Al Amawi aliyekuwa akishikiliwa na polisi baada ya kushukiwa kutuma vifurushi viwili vilivyokuwa na mabomu, ambavyo vilikamatwa katika ndege mbili za mizigo nchini Uingereza na Dubai wiki iliyopita.

Image caption Ofisi ya UPS Yemen

Mwanafunzi huyo alikamatwa siku ya Jumamosi pamoja na mama yake, lakini maafisa wa serikali ya nchi hiyo wamesema imebainika kuwa jina na anwani ya Bi Semawi, ilikuwa imeibiwa na kutumiwa na wahalifu.

Mwandishi wa BBC wa Mashariki ya Kati amesema utawala wa Yemen sasa unanamsaka mshukiwa aliyetengeneza mabomu hayo Ibrahim Hassan al Aziri, raia wa Saudi Arabia anayeishi nchini humo. Mshukiwa huyo anaripotiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la al Qaeda.