Sudan imekiri kuuawa kwa wanajeshi wake

Wapiganaji wa JEM
Image caption Wapiganaji wa JEM

Watu kadhaa wameuawa kwenye makabiliano makali kati ya jeshi la serikali ya Sudan na kundi moja la waasi katika jimbo la Darfur, huku kila upande likidai ushindi.

Waasi wa kundi la Justice and Equality Movement (JEM) limekabiliana na jeshi la serikali Kusini mwa Darfur, eneo ambalo ni mbali sana kutoka kwa ngome yao Kaskazini Magharibi mwa Darfur.

Maafisa wa serikali nchini humo wanasema wanajeshi kadhaa wa serikali waliuawa.

Mwandishi wa BBC mjini Khartoum anasema sio kawaida ya serikali ya nchi hiyo kukubali kuuwawa kwa wanajeshi.