Mashirika ya ndege yasimamisha shughuli

Injini iliyoathirika
Image caption Hakuna abiria aliyejeruhiwa

Shirika la Ndege la Australia, Qantas limesimamisha jumlka ya ndege zake sita muundo wa aina ya Airbus A380 kufuatia tukio la moja ya ndege zake kulazimika kutua kwa dharura.

Safari ya Qantas namba QF32 ilipatwa na matatizo ya Injini mda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Singapore ikiwa njiani kwenda Sydney.

Mlipuko ulitokea upande wa Injini moja, kwa mujibu wa abiria mmoja aliyezungumza na BBC,na vipande vyake vilipatikana kwenye kisiwa.

Kutokana na tukio hilo Shirika la ndege la Singapore nalo likasema kuwa linasimamisha safari za ndege zake zote za muundo wa A380 hadi uchunguzi wa kiufundi ufanywe.

Watengenezaji maarufu wa Injini za ndege Rolls-Royce wamesema kuwa wameanza mchakato wa kuchunguza muundo wa Injini aina ya 20 A380 katika ndege zilizopo - katika Mashirika mbalimbali, la Qantas, Singapore na Lufthansa, mashirika yanayotumia Injini aina ya Trent 900.

Miundo mingine aina ya 17 A380 zinazoendelea na huduma kwa mashirika ya ndege ya Ufaransa na Emirates hutumia aina tofauti ya Injini.

Uchunguzi utafanywa na Shirika la usalama wa safari za Anga la Ulaya(EASA) ambalo Ripoti yake ya mwezi Agosti iligusia uwezekano wa matatizo ya Injini kutokea. Hata hivyo hakuna ushahidi kuwa kuna uhusiano na tukio la hivi sasa.

'wasiwasi mkubwa' Taarifa ya Qantas imesema kuwa safari ya QF32, ikiwa na abiria 433 na wahudumu 26, ilipatwa na matatizo ya Injini ikiwa juu ya anga ya Indonesia ya magharibi mda mfupi baada ya kuondoka uwanja wa Singapore usiku wa manane.Hakuna abiria wala mhudumu wa ndege hiyo aliyejeruhiwa.