Ndege iliyokuwa na abiria 68 yaanguka Cuba

Ndege ya Cuba
Image caption Ndege ya Cuba

Ndege moja ya abiria nchini Cuba imeaguka katikati mwa nchi hiyo ikiwa imebeba takriban abiria 68.

Kwa mujibu wa shirika la habari la nchi hiyo, ndege hiyo ni mali ya shirika la ndege la Caribbean, inayomilikiwa na serikali.

Ndege hiyo ilikuwa inatoka mji wa Santiago de Cuba, Mashariki mwa nchi hiyo, ikielekea mji mkuu Havana wakati ilipoanguka.

Raia wa kigeni 28 ni miongoni mwa abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Hakuna ripoti yoyote kuhusu manusura wa ajali hiyo.