Raia waambiwa waondoke kambi za muda-Haiti

Wamama na watoto wakihamisha kutoka kambi moja nchini Haiti
Image caption Wamama na watoto wakihamisha kutoka kambi moja nchini Haiti

Serikali ya Haiti imetoa wito kwa maelfu ya raia wake ambao wanaishi katika kambi za muda kuondoka kabla ya kimbunga kupiga kisiwa hicho.

Kimbunga kiitwacho TOMAS kinatarajiwa kupiga kisiwa hicho baadaye hii leo.

Watabiri wa hali ya hewa wameonya kuwa kimbunga hicho huenda kikaharibu kambi zote za muda zilizojengwa kwa hema.

Maelfu ya raia wa nchi hiyo wanaishi katika kambi hizo za muda tangu kutokea kwa tetemeko la ardhi nchini humo mwezi januari mwaka huu.

Image caption Watu wanaoishi kambi za muda Haiti

Hatahivyo, licha ya onyo hilo wengi wao wamekataa kuondoka, wakisema kwamba hawana mahala pengine pa kuhamia.

Mashirika ya kutoa misaada yanajitahidi kupata na kuandaa makao ya dharura kwa raia hao kabla ya kimbunga hicho cha Thomas kugonga.

Watu kumi na wanne tayari wameuawa na kimbunga hicho katika eneo la Saint Lucia katika maeneo ya Caribbean.