Kikwete atangazwa rais wa Tanzania

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete
Image caption Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete

Mgombea wa urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa Tanzania uliofanyika siku ya Jumapili.

Bw Kikwete amepata jumla ya kura 5,276,827 ambazo ni sawa na asilimia 61.17 ya kura zote zilizopigwa.

Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dr Wilbrod Slaa amepata ushindi wa pili kwa kura milioni mbili na laki mbili, sawa na asilimia 26.34.

Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF, ameambulia nafasi ya tatu baada ya kukusanya kura 695,668 ambazo ni mgao wa asilimia nane.

Wagombea wengine na asilimia ya kura zao ni kama ifuatavyo Peter Mziray, asilimia 1.12.

Hashim Rungwe asilimia 0.31, Mutamwega Mgahywa asilimia 0.20 na Fahmi Dovutwa asilimia 0.15.

Bw Kikwete ataapishwa kesho kutumikia awamu ya pili kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.