Obama awasili India

Obama awasili India
Image caption Obama awasili India

Rais Obama amewasili nchini India ikiwa ni sehemu ya kwanza ya ziara yake ya siku kumi ya mataifa manne barani Asia.

Rais atawahutubia wakuu wa makampuni ya kibiashara ya India na Marekani katika mji mkuu wa kibiashara wa India, Mumbai, ikiwa ni jaribio la kukuza uhusiano wa kibiashara beina ya nchi hizo mbili.

Pia atazuru eneo la makumbusho la watu mia moja na sitini na sita waliouwawa mwaka wa 2008, katika mashambulizi ya wanamgambo wa kiislam walio na makao yao nchini Pakistan.

Kabla ya ziara ya Bw Obama, India imeonyesha wasiwasi wake juu ya kiasi cha silaha ambacho Marekani inaipatia Pakistan.