Uchaguzi wa marudio wafanyika Guinea

Wanajeshi wa Guinea
Image caption Wanajeshi wa Guinea

Wananchi katika taifa lililo Afrika Magharibi la Guinea wanaelekea kwenye vituo vya kupigia kura kwa marudio ya uchaguzi wa urais ambao unatajwa kama uchaguzi wa kwanza huru kufanyika nchini humo katika kipindi cha miaka hamsini.

Wagombea wanaoshiriki uchaguzi huo, Cellou Dalein Diallo na Alpha Conde, ni kutoka makabila mawili makuu nchini humo.

Wafuasi wao wamekuwa wakipambana tangu kufanyika kwa duru ya kwanza ya uchaguzi mwezi June, na duru ya pili kuahirishwa.

Guinea imekuwa ikiongozwa tangu mwezi January na serikali ya muda ya General Sekouba Konate, aliyechukua mamlaka kutoka kwa viongozi wa mapinduzi ya mwaka 2008.