Maharamia Wakisomali wapokea dola milioni tisa

Ndege ikidondosha fedha kwa maharamia
Image caption Ndege ikidondosha fedha kwa maharamia

Kiasi kikubwa cha fedha za kikombozi katika historia kimelipwa kwa maharamia Wakisomali ili kuaichilia huru meli inayomilikiwa na Korea Kusini.

Maharamia walipokea kiasi cha dola millioni tisa ili waachiliea meli ya Samho Dream, ya Korea Kusini iliyotekwa nyara mwezi April ikiwa imebeba mafuta ikitokea Iraq kuelekea Marekani.

Katika tukio lingine, maharamia walilipwa dola millioni tatu ili kuiachilia meli inayobeba chemikali ya Golden Blessing,inayomilikiwa na Uchina, na yenye usajili wake nchini Singapore.

Mwandishi wa BBC anasema kiwango cha malipo ya fedha za kikombozi kinaelekea kubadili kanuni linapokuja suala la kuziachilia huru meli zinazoshikiliwa na maharamia.

Meli nyingine 25 baado ziko mikononi mwa maharamia Wakisomali nje ya pwani ya Somalia.