Rais Obama azuru India

Rais wa Marekani Barack Obama ameelezea umuhimu wa kuwepo uhusiano imara na wenye faida kati ya nchi yake na India.

Image caption Rais Obama na waziri mkuu wa India Manmohan Singh.

Rais Obama na mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh, wameahidi kushirikiana katika vita dhidi ya ugaidi.

Rais huyo wa Marekani ameutaja uhusiano kati ya nchi yake na India umeimarika zaidi katika karne ya 21.

Amesema amefanya mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo kuhusu hali ya eneo la mashariki mwa Asia, ambalo wengi wanaamini linajumuisha China na pia Afghanistan.

Marekani halikadhalika imeondoa vikwazo dhidi ya shirika la ulinzi la India kufanya biashara na Marekani. Vikwazo hivyo viliwekwa mwaka 1998, baada ya India kufanya majaribio ya Nyuklia.

Nchi hizo zimekubaliana kuimarisha usalama, hasa katika viwanja vya ndege na bandari.