Wanahabari 10 watiwa nguvuni Libya

Image caption Wanahabari wakamtwa Libya

Ripoti kutoka nchini Libya zinasema kuwa maafisa wamewatia nguvuni waandishi wa habari kumi wa shirika la Habari la Libya Press ambalo linathibitiwa na mmoja wa wanawe wa kiume wa kiongozi wa taifa hilo, Muammar Gaddafi.

Chama cha waandishi wa habari nchini Libya kimesema waandishi hao, wanawake 4 na wanaume 6 wanazuiliwa kwa kukosoa uongozi wa taifa hilo.

Waandishi wa habari wamesema mwana wa kiume wa bwana Muammar Gaddafi, Saif al-Islam, anaonekana kuwa mwana mageuzi ambaye ametoa sauti ya kuikosoa serikali katika miezi ya hivi karibuni.