Bush atetea mbinu za kuwatesa wafungwa

Aliyekuwa Rais wa Marekani, George W Bush, ametetea maamuzi yake yaliyosababisha utata mkubwa wakati wa mahojiano yake ya kwanza kwenye televisheni tangu aondoke madarakani.

Image caption George Bush

Akizungumza kweye kituo cha televisheni cha Marekani cha NBC, Bw Bush alitetea mbinu ya kuwatesa wafungwa kwa kuwazamisha ndani ya maji wakati walipokuwa wakihojiwa, akisema ilisaidia kuokoa maisha na kuzuia mashambulio ya kigaidi.

Amesema uamuzi wake wa kuvamia Iraq haukuwa na kasoro na dunia kwa sasa ni salama zaidi bila Saddam Hussein.

Pia alitetea uamuzi wake wa kuyanusuru mabenki ya Marekani yaliyoporomoka kutokana na mdororo wa kiuchumi duniani.

Bwana Bush amesema anatarajia kuwa historia itatambua mafanikio yake ingawa atakuwa ameaga dunia kabla swala hilo kutokea.