Cameron azungumzia siasa na uchumi China

Waziri Mkuu wa Uingereza , David Cameron, ametoa hotuba muhimu wakati akimaliza ziara yake nchini China, ambapo amegusia masuala ya uchumi na uhuru wa kisiasa.

Image caption David Cameron akiwa China

Akizungumza na wanafunzi wa chuo kikuu, Bw Cameron amesema China inaendelea kuimarisha nafasi yake kama taifa lenye ushawishi mkubwa duniani.

Amesema Uingereza haitaki kuifundisha China kuhusu haki za binadam, lakini ni muhimu kwa China kuzungumzia swala hilo na mataifa yenye uhusiano wa karibu.