Rais Da Silva wa Brasil azuru Mozambique

Image caption Rais anayeondoka wa Brasil Lula Da Silva

Rais wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, leo anazuru Msumbiji ambapo atatembelea kiwanda kinachotengeneza dawa za kufubaza virusi vya ukimwi ambacho kinajengwa kwa msaada wa serikali ya Brazil.

Kitakapofunguliwa mwaka ujao kiwanda hicho kinatarajiwa kuwa cha kwanza kumilikiwa na umma barani Afrika, ambacho kinatengeneza dawa za kukabiliana na makali ya ugonjwa wa ukimwi.

Rais huyo wa Brazil anatarajiwa pia kuzindua mpango wa maendeleo ya kilimo na kujadili uhusiano wa kibiashara katika ziara yake ya siku mbili nchini humo.