Maharamia wateka meli ya Wachina

China imesema maharamia wameiteka meli ya mizigo katika bahari ya Uarabuni iliyobebea mabaharia 29 raia wa China.

Image caption Maharamia wa Kisomali

Vyombo vya habari vya serikali ya China vimesema wamiliki wa meli hiyo yenye usajili wa Panana, walisema meli hiyo ilikuwa ikielekezwa upande wa Somalia na maharamia hao.

Shirika la Kimataifa la Shughuli za Bahari, limesema maharamia Wakisomali wanashikilia meli ishirini zikiwa na wafanyakazi zaidi ya mia nne wakitaka kulipwa fedha za kikombozi.