Watu wanane wauawa Afghanistan kwa bomu

Shambulio la bomu kaskazini mwa Afghanistan limewauwa watu takriban ya wanane na kujeruhi wengine 18.

Image caption Shambulio la bomu Kunduz

Maafisa katika eneo hilo wamesema bomu lililofichwa katika pikipiki lililipuka eneo lenye watu wengi sokoni katika mji uliopo katika jimbo la Kunduz .

Katika tukio, waasi walishambulia kituo cha kijeshi karibu na uwanja wa ndege wa Jalalabad mashariki mwa Afghanistan.

Kundi la Taleban limekiri kuhusika na shambulio hilo.

Jeshi la Afghanistan na wanajeshi wa kimataifa wamesema waliwauwa waasi wanane wakati wakijibu shambulio hilo katika mapambano makali yaliyodumu kwa saa mbili.