Sebastian Vettel ashinda mbio za F1

Vettel
Image caption Sebastian Vettel

Sebastian Vittel wa Ujerumani ameshinda mbio za magari ya langalanga, baada ya pia kushinda mbio za mwisho za Abu Dhabi.

Vettel amepata jumla ya pointi 256, akifuatiwa na Fernando Alonso wa Ferrari aliyepata pointi 252.

Mark Webber wa Red Bull amemaliza katika nafasi ya tatu akiwa na pointi 242, huku Lewis Hamilton wa McLaren Mercedes amemaliza katika nafasi ya nne akiwa na pointi 240.