Talabani kutoidhinisha kunyongwa Aziz

Rais wa Iraqi, Jalal Talabani, amesema hataidhinisha amri ya kunyongwa aliyekuwa naibu wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Tariq Aziz wakati wa utawala wa kiongozi wa kiimla Saddam Hussein.

Image caption Tariq Aziz

Tariq Aziz aliyetambulika sana kama mtetezi wa Sadam Hussein kimataifa, alihukumiwa kifo na mahakama kuu nchini humo mwezi uliopita kwa tuhuma za kuhusika na mauaji pamoja na mat ya maelfu ya wafuasi wa vyama vya Kiislamu nchini humo.

Rais Talabani amesema hataidhinisha kuuawa kwa Tariq Aziz ambaye ni Mkristo kwa kuwa ni mzee na anamhurumia kwa masaibu yaliomkabili kwa muda mrefu .