Mizengo Pinda waziri mkuu tena Tanzania

Image caption Mizengo Pinda

Mizengo Pinga atajwa kuendelea kuwa waziri mkuu wa Tanzania. Baada ya jina lake kupendekezwa na rais Jakaya Kikwete, na kusomwa bungeni na spika wa Bunge, Anna makinda, wabunge walimpigia kura kumuidhinisha. Bw Pinda amepata zaidi ya asilimia 80 ya kura zilizopigwa. Naibu spika wa bunge amechaguliwa Job Ndugay kutoka CCM.