Rwanda- Paul Rusesabagina akamatwe

Paul Rusesabagina
Image caption Paul Rusesabagina

Mtayarishi wa filamu maarufu iitwayo Hotel Rwanda, Paul Rusesabagina, ametuhumiwa na serikali ya Rwanda kufadhili mauaji ya kimbari ya mwaka wa 1994.

Raia huyo wa Rwanda, alipata sifa ya kimataifa baada ya kutayarisha filamu hiyo iliyoonyesha matukio ya mauaji ya kimbari nchini humo 1994 .

Serikali ya Rwanda imedai Rusesabagina ni mfadhili wa kundi la waasi wa FDLR wanaotuhumiwa kutekeleza mauaji hayo na imewasilisha ombi kwa Marekani na Ubeljiji, kumkamata raia huyo na kumfungulia mashtaka.

Inasemekana jitihada zake zilisaidia kuokoa maisha ya raia wa Kitutsi waliokimbilia katika hotel hiyo kutafuta hifadhi.

Image caption Kanda ya filamu ya Hotel Rwanda

Lakini serikali ya nchi hiyo imekanusha madai hayo.

Mwendesha mashtaka mkuu wa Rwanda, Martin Ngoga amesema sababu ya kuomba mataifa ya Marekani na Ubelgiji, kumfuatilia mshukiwa huyo, ni kuwa mashtaka yanayomkabili yalitekelezwa katika mataifa hayo.

Ngoga amesema serikali ya nchi hiyo ina ushahidi wa kutosha dhidi ya Paul Rusesabagina.

Mshukiwa huyo amenukuliwa akisema kuwa hana wasi wasi wowote kufika katika mahakama yoyote nje ya Rwanda kujibu mashtaka hayo kwani anaamini kuwa hana hatia.