Hali tete mgodini New Zealand

Watu ishirini na tisa waliokwama mgodi nchini NewZealand hawataokolewa kwa sasa. Juhudi za kuwaokoa watu hao huenda zikaanza kesho.

Image caption Mgodi New Zealand

Uchunguzi uliofanywa na wataalam, umegundua kuwepo kwa kiwango kikubwa kwa gesi hatari kwenye mgodi huo. Watu hao wamekwama katika mgodi huo tangu siku ya Ijumaa baada ya kutokea mlipuko.

Baadhi ya waliokwama ni kijana mwenye umri wa miaka kumi na saba na mzee wa miaka sitini na miwili.

Kuna raia wawili wa Australia na wawili wa Uingereza. Tayari kikosi cha wataalam kutoka Australia kimewasilini nchini humo kusaidia juhudi za uokoaji.