Mkutano wa SADC wajadili mizozo

Mkutano wa SADC unaofanyika Botswana unatoa umuhimu wa kwanza kwa hali ya taharuki inayotanda Madagascar na Zimbabwe.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma atawasilisha taarifa kuhusu hatua zinazopigwa na serikali ya muungano nchini Zimbabwe.

Mpango wa kugawana madaraka kati ya Rais Robert Mugabe na Waziri Mkuu Morgan Tsvangarai umekuwa ukiyumba huku kukiwa na hofu ya kutokea kwa mivutano na hata ghasia za kisiasa, huku nchi hiyo ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu.