Kesi ya kiongozi wa DRC Bemba kuanza leo

Kesi dhidi ya kiongozi wa zamani wa kundi la waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jean Pierre Bemba, inatazamiwa kuanza leo jumatatu katika mahakama ya kimataifa ya Uhalifu wa kivita iliyopo mjini Hague uholanzi.

Bwana Bemba anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu kutokana na majukumu yake ya kuwaongoza wapiganaji kuwaua na kuwatesa raia katika taifa jirani la jamhuri ya Afrika ya kati mwaka 2002 na mwaka 2003.

Akiwa amewahi kuhudumu kama makamu wa rais wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, bwana Bemba, ndiye mtu wa kwanza aliyekuwa na ushawishi mkubwa kuhukumiwa katika mahakama ya ICC.

Viongozi wa mashtaka wamedai kuwa hakufanya lolote kuwazuia wanajeshi wake kutumia ubakaji kama silahaa ya vita madai ambayo Aimé Kilolo, ambayo ni mmoja wa mawakili wa bwana Bemba ameyakanusha.