Kesi ya kiongozi wa DRC Bemba kuanza leo

Pierre Bemba
Image caption Bwana Jean Pierre Bemba

Kesi ya aliyekuwa kiongozi wa kundi la waasi katika Jamhuri ya demokrasia ya Congo Jean Pierre Bemba inatarajiwa kuanza baadaye leo,mjini the Hague,Uholanzi.

Bemba anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binaadamu.

Haya yanahusiana na mambo ambayo makundi yake ya wanamgambo yalifanya dhidi ya raia katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati mwaka 2002 and 2003.

Bemba alikuwa makamu wa rais wa Congo, na ni kiongozi wa ngazi za juu kufikishwa katika mahakama ya kimataifa ya ICC.

Upande wa mashtaka unadai kuwa alishindwa kudhibiti vikosi vyake wakati vilipotekeleza ubakaji kama silaha moja ya vita.

Bwana Bemba amekanusha mashtaka hayo yanayomkabili.