Polisi wahofia mlipuko New Zealand

mgodi wa New Zealand
Image caption Picha za awali za mlipuko uliotokea zimechapishwa lakini polisi wanahofia usalama wa eneo hilo

Wafanyakazi wa mashirika ya uokoaji nchini New Zealand wamechapisha picha zilizonaswa na mtambo wa roboti zinazoonyesha mlipuko mkubwa uliotokea ndani ya mgodi wa Pike River.

Kiongozi wa shughuli za uokozi superintendent Gary Knowles, amesema sio salama kuwatuma waokoaji ndani ya mgodi huo ikiwa haijabainika kuwa gesi inayotoka ndani ina sumu au la.

Majaribio ya kutathmini hali katika mgodi huo yanaendelea baada ya mtambo wa pili wa roboti kutumwa ndani ya mgodi huo baada ya ule wa kwanza kuharibika.

Polisi wamesema wana matumaini ya kuwapata wachimba migodi 29 waliokwama ndani tangu ijumaa wakiwa hai ingawa wamejiandaa kuwapata wengine wakiwa wamefariki dunia.