Chelsea yailaza MSK Zilina mabao 2-0

Damu changa za vijana wa Chelsea ziliiwezesha timu hiyo kuvuna pointi tatu katika kundi lao la F baada ya kuwa nyuma kwa bao moja dhidi ya MSK Zilina na kuibuka kwa usindi wa mabao 2-0.

Zilina waliwashtua Chelsea baada ya Babatounde Bello kugongea moja mbili na Robert Jez na kufumua mkwaju mkali wavuni.

Lakini hekaheka zilizooneshwa na Chelsea, zilifanikiwa baada ya Daniel Sturridge kupachika bao baada ya kupokea krosi ya mbali ya Salomon Kalou.

Chelsea ilizidi kushambulia na kujipatia bao la pili baada ya Didier Drogba na Patrick van Aanholt kugongea na hatimaye, Florent Malouda kumalizia kazi.

The Blues tayari wamejihakikishia nafasi ya kucheza hatua ya mtoano ya timu 16 kuwania Ubingwa wa Ulaya hata kabla ya mechi hiyo, lakini hata hivyo mechi hiyo ilikuwa na umuhimu kwao kutokana na kucheza ovyo katika michezo ya ligi hivi karibuni walipopoteza mechi tatu, vile vile kutimuliwa kwa meneja msaidizi Ray Wilkins na suala kuhusu hatma ya meneja Carlo Ancelotti.