Kikwete atangaza baraza la mawaziri

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania ametangaza baraza lake jipya la mawaziri kukamilisha uundaji wa serikali tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.

Image caption Kikwete amewaacha mawaziri kadhaa wa zamani na kuteua sura mpya kama vile Profesa Anna Tibaijuka.

Rais Kikwete alitaja serikali yake mbele ya waandishi wa habari katika shughuli iliyofanyika Ikulu mjini Dar Es Salaam, akibainisha kuwa hakuna mabadiliko makubwa katika idadi ya wizara, zipo jumla ya wizara 26.

Sura mpya kadhaa zimetajwa ikiwa ni pamoja na Profesa Anna Tibaijuka atakayesimamia wizara ya ardhi na makazi.Profesa Tibaijuka alikuwa mkurugunzi mkuu wa shirika la makazi la Umoja wa Mataifa kabla ya kujiuzulu na kwenda kugombania ubunge jimbo la Muleba Kusini.

Waziri aliyetajwa kinyume na maelezo ya wachambuzi wengi wa kisiasa ni Samuel Sitta, baada ya kuondolewa kiti cha spika wa bunge la Muungano, sasa anakuwa Waziri wa maswala ya Afrika Mashariki.

Mawaziri wengi wa serikali iliyopitwa wamerejeshwa tena katika majukumu waliyokuwa nayo awali kama vile Bernard Membe atakayeendelea kusimamia mambo ya nje.Mustapha Mkullo anarudi kuongoza wizara ya fedha.

Marekebisho kadhaa ameyataja Rais Kikwete katika uundaji wa baraza lake kuwa idara ya vijana imeondolewa kutoka wizara ya kazi na kuhamishiwa wizara ya habari na michezo.

Wanasiasa kadhaa waliokuwa katika serikali iliyopita wameachwa, baadhi yao ni wasomi maarufu kama Profesa Peter Msola aliyekuwa Sayansi na Teknolojia, Profesa Juma Kapuya aliyekuwa Kazi na Profesa David Mwakyusa aliyekuwa afya, mwingine ni kada wa chama kama John Chiligati aliyeachwa wizara ya ardhi.

Waziri hao wataapishwa siku ya Jumamosi katika viwanja vya Ikulu ya Dar Es Salaam.

Orodha kamili ya mawaziri na manaibu waziri hii hapa chini.

Namba Ofisi/Wizara Waziri Naibu Waziri
1. Ofisi ya Rais 1. Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais – Utawala BoraMathias Chikawe2. Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais – Mahusiano na UratibuStephen Wassira
2. Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Hawa Ghasia
3. Ofisi ya Makamu wa Rais 1. MuunganoSamia Suluhu2. MazingiraDr. Terezya Luoga Hovisa
4. Ofisi ya Waziri Mkuu 1. Sera, Uratibu na BungeWilliam Lukuvi2.Uwekezaji na UwezeshajiDr. Mary Nagu
5. Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Mkuchika 1.Aggrey Mwanri2. Kassim Majaliwa
6. Wizara ya Fedha Mustapha Mkulo 1. Gregory Teu2. Pereira Ame Silima
7. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Shamsi Vuai Nahodha Khamis Kagasheki
8. Wizara ya Katiba na Sheria Celina Kombani
9. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe Mahadhi Juma Mahadhi
10. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dr. Hussein Mwinyi
11. Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dr. Mathayo David Mathayo Benedict Ole Nangoro
12. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mnyaa Mbarawa Charles Kitwanga
13. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka Goodluck Ole Madeye
14. Wizara ya Maliasili na Utalii Ezekiel Maige
15. Wizara ya Nishati na Madini William Ngeleja Adam Kigoma Malima
16. Wizara ya Ujenzi Dr. John Magufuli Dr. Harrison Mwakyembe
17. Wizara ya Uchukuzi Omari Nundu Athumani Mfutakamba
18. Wizara ya Viwanda na Biashara Dr. Cyril Chami Lazaro Nyalandu
19. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa Philipo Mulugo
20. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Haji Hussein Mpanda Dr. Lucy Nkya
21. Wizara ya Kazi na Ajira Gaudensia Kabaka Makongoro Mahanga
22. Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Sophia Simba Umi Ali Mwalimu
23. Wizara ya Habari, Vijana na Michezo Emmanuel Nchimbi Dr. Fenella Mukangara
24. Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta Dr. Abdallah Juma Abdallah
25. Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Prof. Jumanne Maghembe Christopher Chiza
26. Wizara ya Maji Prof. Mark Mwandosya Eng. Gerson Lwinge