Waziri mkuu wa Iraq kuunda serikali

Waziri mkuu Nouri al-Maliki
Image caption Bw Maliki ameruhusiwa kuunda serikali mpya

Waziri mkuu wa Iraq, Nouri al-Maliki, ameteuliwa kuunda serikali mpya.

Hatua hiyo inaondoa hali ya wasiwasi wa kisiasa iliokuwepo kwa kipindi cha miezi minane, tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Iraq uliokuwa na utata.

Bw Maliki ana siku 32 kujadiliana kuhusu ni vipi atagawa madaraka miongoni mwa baraza la mawaziri, kwa kushirikiana na vyama vyengine.

Serikali hiyo inatazamiwa kuvijumuisha vyama vyote vikuu nchini Iraq, na madhehebu yote ya Kiislamu; Washia, Wasuni na Wakurdi.

Kuteuliwa rasmi kwa Bw Malik ni kati ya utaratibu ulioafikiwa mapema mwezi huu, wa kugawanya madaraka, na ambao utamwezesha pia kuchuua hatamu za uongozi kwa muhula wa pili.