Bashir kuhudhuria mkutano Afrika, Ulaya

Aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki ametangaza kuwa Rais wa Sudan, Jenerali Omar al-Bashir, anayetakiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu, atahudhuria mkutano wa viongozi wa Africa na Ulaya utakaofanyika wiki hii.

Image caption Jenerali Omar al-Bashir

Mkutano huo unafanyika nchini Libya ambayo si mwanachama wa ICC na kwa hivyo haiwajibiki kumkamata Rais Bashir.

Lakini waandishi wa habari wanasema kuhudhuria kwake kutasabisha tatizo la kidiplomasia kwa wawakilishi wa Muungano wa Ulaya ambao wana wajibu wa kutekeleza hati za kukamatwa kwa washukiwa zinazotolewa na mahakama hiyo.