China yawaza uhusiano na Korea Kaskazini

Ripoti za mawasiliano ya siri kati ya balozi za Marekani zilizochapishwa kwenye mtandao wa Wiki Leaks, zinaashiria viongozi wa China wamekuwa wakifikiria ni nini kitafanyika iwapo uhusiano kati yao na Korea Kaskazini utasambaratika.

Image caption Kiongozi wa Korea Kaskazini alipokuwa China

Afisa mmoja mwandamizi wa serikali ya Korea Kusini, aliwanukuu wawakilishi wawili wa China wakisema, Beijing itakuwa tayari kukubali ushirikiano wa karibu kati ya Korea Kusini na Kaskazini bora tu usihatarishe uhusiano uliopo na China.

Afisa mwingine wa China alinukuliwa akisema Korea Kaskazini imeedekezwa sana, matamshi yanayoonesha nchi hiyo imechoshwa na jinsi taifa hilo linavyoendeleza shughuli zake.

Kufikia sasa hata hivyo China imesema machache kuhusiana na kuchapishwa kwa nyaraka hizo za siri kwenye mtandao wa Wikileaks, lakini imekuwa ikiishinikiza Marekani kuhakikisha inachukua hatua mwafaka.