Wananchi wa Misri wapiga kura

Wananchi wa Misri leo wanapiga kura katika uchaguzi wa bunge katika shughuli ambayo tayari imekumbwa na ghasia kati ya wapinzani na vikosi vya usalama.

Image caption Wamisri wakipiga kura

Chama tawala cha Rais Hosni Mubarak kinatarajiwa kushinda kwa urahisi, lakini jambo muhimu ambalo wengi wanataka kufahamu ni ikiwa chama kikubwa cha upinzani cha Muslim Brotherhood, kinaweza kudhibiti nafasi yake hiyo ya kuwa chama kikuu cha kambi ya upinzani.

Chama hicho kimepigwa marufuku nchini Misri, kwa hivyo wafuasi wake wanashiriki uchaguzi wakiwa wagombea huru.