Pakistan wakanusha madai ya Wikileaks

Wizara ya Mambo ya Nje nchini Pakistan imekanusha madai kuwa Marekani inahusika na shughuli ya kusafirisha madini yaliyorotubishwa ya uranium kutoka katika viwanda vyake vya Nukilia.

Image caption Ripoti ya Wikileaks

Msemaji wa wizara hiyo ameiambia BBC, habari hizo zilijitokeza kwenye nyaraka zilizochapishwa na mtandao wa Wikileaks.

Nyaraka hizo zimeonyesha matamshi yaliyotolewa na mfalme Abdullah wa Saudi Arabi kuhusu Rais wa nchi hiyo Asif Zardari.